HAKIKISHA UNANENA KWA LUGHA YA ROHO MTAKATIFU (Bofya hapa uangalie video)
HAKIKISHA
UNANENA KWA LUGHA YA ROHO MTAKATIFU
Kimsingi
kuna lugha za aina mbalimbali:
1.
Lugha za kibinadamu – lugha ya kabila lako na ulizosomea
1 Wakorintho 13:1 “Nijaposema
kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na
upatu uvumao.”
Mwa 11:9 “Kwa sababu
hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya
dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”
Si lugha inayotosha katika kujieleza kwa Mungu. Ni matokeo ya Babeli.
2.
Lugha za mapepo
Lk 4:3 “Ibilisi
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.”
3.
Lugha ya Roho Mtakatifu – kunena kwa lugha (kuongea na Mungu)
1 Wakorintho 14:39 “Kwa
ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha.”
4.
Aina za lugha (moja ya karama za Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa) –
kuongea na kanisa – sio kila mtu anapewa (inahitaji kutafsiriwa)
1 Kor 12:10 “na
mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho;
mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha.”
5.
Lugha ya mazoea – Aliwahi kupewa kunena kwa lugha lakini Roho hayuko ndani yake
tena.
1 Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe
Roho.” Hapati maneno tofauti kulingana na maombi aidha kwa kutomruhusu Roho
au kuishi kwa mazoea.
Ufafanuzi kidogo kuhusu KUNENA KWA LUGHA
1. Ni
moja ya ishara za waaminio – hivyo tusiibeze
Marko 16:17,18 “Na
ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema
kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru
kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
2. Mtu
anayenena kwa lugha anaongea na Mungu (sio watu) -
1 Kor 14:2 “Maana
yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna
asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho
yake.”
3.
Kunena kwa lugha ni maombi ya rohoni na sio mwilini
1 Kor 14:14 “Maana
nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.”
4.
Ukinena kwa lugha unashukuru vyema zaidi (ingawa humjengi mwingine)
1 Kor 14:17 “Maana
ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi.”
Kama hujaona ajali iliyokuwa inataka kutokea hutaweza
kumshukuru Mungu lakini kupitia Roho Mtakatifu unaweza kushukuru kwa kunena kwa
lugha. Roho wa Mungu anajua yote hata yale ambayo huyajui kibinafsi.
5.
Kunena kwa lugha ni muhimu kibinafsi na sio kwa wengine
1 Kor 14:18,19 “Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote; lakini katika kanisa napenda kunena maneno
matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno
kumi elfu kwa lugha.”
Mtume
Paulo anakiri kwamba alikuwa ananena kwa lugha kuliko watu wote Korintho
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unipe roho ya kujifunza ili nisibeze
utendaji wa Roho Wako.
2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuchochea uwezo ulionipa ili
ninufaike na utendaji wa Roho ndani yangu.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao).

