JISHUSHE NA KUFURAHIA MAENDELEO YA WENGINE (Bofya uangalie video)
JISHUSHE
NA KUFURAHIA MAENDELEO YA WENGINE
Usipende
kuonekana unajua kila kitu. Uwe na roho ya kujifunza kwa wengine bila unafiki.
Wafilipi 2:3,5-8 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa
unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 5 Iweni
na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya
Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu,
akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana
umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya
msalaba.
Mwanzo
wa anguko ni kuwa na kiburi
Mit 16:18 “Kiburi
hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.”
Ujuzi huleta majivuno
1 Kor 8:1,2 “Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.”
Unapooona umefanikiwa, jisifu ndani ya nafsi yako mwenyewe
Gal 6:3,4 “Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.”
Mfano mzuri wa kujifunza unyenyekevu
Mt 3:11 “Kweli mimi
nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu
kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa
Roho Mtakatifu na kwa moto.”
Yohana hakukasirika Yesu alipomchukulia washirika na kupata umaarufu kuliko yeye. Alijitambua Yeye ni nani na mipaka ya huduma yake. Yn 3:26-30 “Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”
Yn 21:17,20-22 “Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu. Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi.”
Petro hakuridhika na kazi aliyopewa. Akataka kujua mambo
yasiyomhusu.
2 The 3:11 “Maana
twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao
wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.” – uwe na shughuli
zako mwenyewe
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba uniondolee roho ya kiburi ili
niwathamini wengine na kuweza kujishusha.
2, Ee Mungu naomba uniwezeshe kukuinua kupitia mafanikio
yangu ili uzidi kujitukuza kupitia maisha yangu.
Dr. Lawi Mshana, +255712924234; Tanzania