Ticker

6/recent/ticker-posts

BARIKIWA KWA MOYO WAKO WA UTOAJI


 BARIKIWA KWA MOYO WAKO WA UTOAJI

Tunashukuru sana kwako uliyehamasika kutuunga mkono katika maono tuliyo nayo kwa ajili ya jamii.
Kuna mdau wa maendeleo ametupatia nguo (mashati, suruali na makoti) na viatu kwa ajili ya programu yetu ya kukabiliana na uhatarishi na majanga (vulnerability and disaster management).
Nadhani hata wewe una vitu nyumbani kwako ambavyo kwa sasa huvitumii ingawa vingeweza kumfaa mtu fulani kama vile kompyuta, TV, fanicha, nguo nk. Mungu ameendelea kubariki mataifa mengine kwa vile wanatoa mitumba wanapobarikiwa kupata vipya.
Mungu atakuongeza kama utaungana nasi kusaidia jamii bila mipaka ya kidini kwa kutoa ulicho nacho au kuahidi kutoa katika mwaka huu mpya. Januari ni mwezi wa kuahidi kumtumikia Mungu kibinafsi kwa vile umeitwa peke yako. Kumbuka tumekuja bila kitu na tutaondoka bila kitu. Tuwekeze kwa ajili ya maisha yetu yajayo.
Dr Lawi Mshana, Beyond Four Walls, 0712-924234