FAHAMU MAANA YA KIFO CHA ROHO (Bofya hapa uangalie video)
FAHAMU
MAANA YA KIFO CHA ROHO
Kifo kiko kwa namna mbili: Kifo cha kimwili na kifo cha
kiroho. Kifo cha kiroho kinaweza kutokea ukiwa bado unatembea duniani na baada
ya kuondoka duniani (kutengwa na Mungu milele).
Hata hivyo kuna watu wamezikwa kimwili lakini bado tarehe
ya kifo walichopangiwa na Mungu haijafika. Hivyo wanatangatanga wakitumwa
kutesa watu (misukule) hapa duniani. Lakini wapo pia watu tunaowaona kimwili
lakini ni watumwa wa kuwanufaisha watu fulani (ndondocha). Muda mwingi
wanachoka kwa vile wanatumikishwa bila kujua.
Ezekieli 13:19 “Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa
ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho
za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao
uongo.”
Shetani
anaweza kuua mwili wako lakini baada ya hapo hawezi lolote tena.
Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na
roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika
jehanum.”
Ili
kuwa salama baada ya maisha haya lazima kuzaliwa mara ya pili (kuzaliwa kiroho)
Yohana 3:4-8 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Kiungo kimoja cha mwili wako kinaweza kukupeleka Jehanum
Mathayo 18:9 “Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.”
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika.”
Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima,
u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum.”
Kama huishi na kuenenda kwa Roho Mtakatifu, uko hatarini
Warumi 8:13 “kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.”
Gal 5:25,26 “Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unipe maisha mapya ili nisiendelee kutumikishwa
na shetani.
2. Ee Mungu naomba unipe ushindi wa dhambi na kuniongoza
kwa Roho wako ili nisije nikapotea milele.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao).