Ticker

6/recent/ticker-posts

TUMETIWA MOYO KWA KUENDELEA KUPATA MARAFIKI WA KUUNGA MKONO MAONO YETU KWA AJILI YA JAMII




 TUMETIWA MOYO KWA KUENDELEA KUPATA MARAFIKI WA KUUNGA MKONO MAONO YETU KWA AJILI YA JAMII

Tumepokea tena msaada wa nguo kutoka kwa mpendwa (mdau wa maendeleo) ambaye ameutuma kutoka mbali. Mpango huu ni wa kupokea misaada ya vitu ambavyo huvitumii sana kwa vile Mungu amekupa vingine. Unaweza kutupatia ile kompyuta, godoro, shuka, shelfu, meza, viti, nguo, vyandarua, spika nk kwa ajili ya vituo vyetu vya kusaidia jamii. Unaweza pia kujitolea KUAZIMA nyumba yako, gari lako, bajaji yako nk kwa ajili ya dharura za watu wanaopata majanga.
Tunajipanga kuwahudumia watu wanaopata dharura za kufanyiwa ukatili ambao kwa muda hawawezi kurudi kwa watu waliowafanyia vitendo hivyo wakati sheria ikichukua mkondo wake. Wengi wanashindwa kuripoti kwamba wamefanyiwa vitendo vibaya kwa vile hakuna makazi ya muda ya kuwahifadhi. Tunawaza tu wahalifu wafungwe lakini tunasahau waathirika watasaidiwaje.
Kadiri unavyotoa ndivyo unavyofungua mlango wa kubarikiwa zaidi. Lakini hata kama hutabarikiwa ukiwa hapa duniani unakuwa umewekeza katika umilele wako badala ya ndugu zako kugawana tu mali zako ukishaondoka duniani. Andaa makazi yako mbinguni kwa kuwasaidia watu ambao hawawezi kukulipa wala kukushukuru.
Luka 6:35 "Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu."
Mungu ayafanye maono yako kuwa halisi kwa vile umeamua kugusa maisha ya watu wanaoishi mazingira hatarishi.
Dr Lawi Mshana, Beyond Four Walls, Korogwe, Tanga, 0712-924234