Ticker

6/recent/ticker-posts

Maoni ya watoto na vijana wa Nitatoboa Initiative



 Maoni ya watoto na vijana wa Nitatoboa Initiative, Korogwe chini ya Beyond Four Walls:

1. Wamesema kwamba ili mtoto na kijana atoboe na kufikia ndoto zake anatakiwa kusoma kwa bidii, kumtanguliza Mungu, kumuomba Mungu, kuwa na malengo, kupata ushauri kwa waliofanikiwa, kuchagua marafiki wazuri, kujali muda, kuepuka vishawishi na kushinda msongo wa mawazo.
2. Wamesema wazazi wawasaidie watoto kufikia ndoto zao kwa kuwa na ratiba nyumbani na kuisimamia, kuwasisitiza watoto wasome kwa bidii, kuwaombea watoto wao, kuwatia moyo, kuwashauri na kuwapatia mahitaji ya msingi.

Pamoja na umri wao mdogo wametoa maoni ya msingi sana hivyo tuyafanyie kazi.