Ticker

6/recent/ticker-posts

Kurejezwa na kuvikwa uwezo (video na maandishi)

KUREJEZWA NA KUVIKWA UWEZO (Bofya hapa kuangalia video)

KUREJEZWA NA KUVIKWA UWEZO

Katika hili wiki la mwisho la mwaka Mungu ana mpango maalum kwako. Badala ya kubadilisha mazingira yako anataka kuanza na wewe mwenyewe. Baadhi yetu tumepata fursa ya kuwa mahali kwa ajili ya kutulia na Bwana.

Zaburi 85:6 Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha, Watu wako wakufurahie

Luka 24:49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Unahitaji kurejezwa maeneo gani?

1. Muda uliopoteza

Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

2. Imani yako

Zaburi 51:12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.

3. Maisha yako

Matendo ya Mitume 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.

Unahitaji kuvikwa uwezo gani?

Mdo 1:8  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

·       Uwezo wa kufanya yasiyowezekana kibinadamu

·       Uwezo wa kutoa maisha yako kwa ajili ya Mungu (Ufunuo wa Yohana 12:11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.)

·       Uwezo wa kuwa na mguso kuanzia pale ulipo hadi mwisho wa dunia (hukuitwa kuandaa mikutano ya Injili hapo ulipo peke yake. Uende zaidi ya Yerusalemu yako.)

Usipotii Mdo 1:8 jiandae kukutana na Mdo 8:1:

Mdo 8:1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.

Tunakukaribisha sana uwe partner wetu katika huduma za kiroho na kijamii kwa mwaka 2024 ili tuendelee kuzitoa bila malipo yoyote. Unaweza kuahidi kiasi chochote kuanzia sh 5,000 kwa mwezi.

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba unihuishe tena ili nisitumike kwa nguvu zangu mwenyewe.

2, Ee Mungu naomba univike uwezo wako ili niweze kujikana kwa ajili Yako

Download na ku-install App ya Lawi Mshana inayopatikana katika blog hii ili upate masomo kwa njia ya maandishi, sauti na video bure.