USHIRIKIANO WA BEYOND FOUR WALLS NA VIKUNDI VYA JAMII UMEANZA RASMI
Leo nimetembelea kikundi cha Manzese Development Group
ambacho kiko kata ya Bagamoyo, Korogwe mjini baada ya kutuandikia barua ya kuomba
tushirikiane katika kukijengea uwezo (empowerment). Baada ya kikao niliungana
nao kutembelea bwawa wanalotarajia kufuga samaki. Naomba wadau wa maendeleo
tuwaunge mkono waweze kujenga kingo sehemu mbili, wapate mbegu bora ya samaki
na utaalamu zaidi kuhusu ufugaji wa samaki.
Inatia moyo kuona hata wamama wazee wameamua kupambana na
utegemezi na umasikini kwa miradi ambayo wanaweza kuitekeleza.
Kumbuka hiki pia ni kipindi ambacho watu binafsi wanaopenda
kushirikiana nasi katika kuhudumia jamii kwa mwaka 2024 wanajaza fomu za ushirikiano
ili tuwatambue. Unapojitolea uwezo wako wa kijamii, kiuchumi na kiakili katika
kugusa maisha ya watu unajitambulisha na kufungua mlango wa kukutana na fursa
mbalimbali. Tunahitaji watu wa kujitolea ujuzi na uzoefu wao (mentors/consultants),
fedha zao, muda wao na nguvu zao.
Ushuhuda: Kuna mwaka niliamua kugusa maisha ya watu 10
wanaoishi na VVU kwa kukutana nao kila mwezi mara moja na kuwapa gilasi ya
maziwa na maneno ya kuwatia moyo. Moyo huu ulisababisha kupata ufadhili wa
kutoa mafunzo kata nzima tofauti na matarajio yangu.
Sina maana kwamba ujitolee ili ulipwe. Lakini unapojitolea
unatambulisha vizuri uwezo wako hata ule ambao haufai kuandika kwenye wasifu
wako wa kuomba kazi.
Karibu sana ushirikiane nasi kwa mwaka 2024.
Dr Lawi Mshana, Mkurugenzi Mtendaji, Beyond Four Walls,
0712-924234



