FAHAMU MUNGU ANAVYOPIMA KAZI NA TAABU YAKO NA KUKUPA THAWABU (Bofya hapa uangalie video)
FAHAMU
MUNGU ANAVYOPIMA KAZI NA TAABU YAKO NA KUKUPA THAWABU
Kuna watu wanaataabika kwa ajili ya Mungu lakini hawazingatii vigezo na masharti aliyoyaweka. Mungu hatatulipa kwa vile TUMECHOKA bali kwa vile TUMEFANYA KAZI YENYE MATOKEO ALIYOKUSUDIA. Kama kazi anatulipa tukiwa bado hapa duniani na zingine katika ufalme ujao.
Mambo anayozingatia
1. Ubora (quality) – mizani itakuwa ni moto
1 Wakorintho 3:12-15 “12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.”
2. Uwezo wa kuzalisha (capacity) – hufanani na mtu mwingine yeyote.
Mathayo 25:15 “Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.”
3. Kumaliza kazi aliyokupa (ukubwa wa kazi)
2 Timotheo 4:7,8 “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”
4. Kudumu kwa kazi yako (sustainability)
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.”
5. Kujituma na bidii (hardworking)
Zaburi 128:2 “Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.” (When you eat the labor of your hands, you shall be happy, and it shall be well with you.)
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unisaidie nijitume kwa kazi na nijali
ubora ili nipokee baraka ulizonipangia.
2. Ee Mungu naomba unijalie kutambua uwezo ulionipa na
kutumia vizuri ili niwe na matokeo mazuri.
3. Ee Mungu naomba unisaidie nitambue ukubwa wa kazi yangu
na jinsi ya kuhakikisha inadumu ili nisifanye kazi ya hasara.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao).
Download na ku-install App ya Lawi Mshana ili upate masomo kwa njia ya maandishi, sauti na video bure

