Ticker

6/recent/ticker-posts

UNACHELEWA KWA VILE HUWEZI KUFANYA MAAMUZI (Video na Maandishi)

UNACHELEWA KWA VILE HUWEZI KUFANYA MAAMUZI (Bofya hapa uangalie video)

UNACHELEWA KWA VILE HUWEZI KUFANYA MAAMUZI

Mungu hakutuumba kama robot bali ametupa utashi. Maisha yetu yanategemea sana uchaguzi tunaoufanya.

Maono: Nimeona mtu anakaribia kupata madhara yanayoepukika kwa vile anachelewa kuamua achukue hatua gani. Ilibidi nitumie nguvu kumvuta ili kumnusuru. Pengine huyo mtu ni wewe!

1. Mazuri na mabaya yako mbele yako – chagua vizuri (hiyo sio kazi ya Mungu)

 Kum 30:19 “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako.

2. Acha kusita-sita (fanya maamuzi makini)

1 Fal 18:21 “Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.

Yak 1:8 “Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

3.  Uwe na nia moja na sio mbili (double-minded)

Yak 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 

4. Amua pamoja na familia yako (pangeni pamoja) 

Yos 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba uniongoze katika kufanya maamuzi ili nisijiingize katika matatizo.

2. Ee Mungu naomba uondoe roho ya kusitasita na kuwa na nia mbili ndani yangu.

3. Ee Mungu naomba uniwezeshe kushirikiana na familia katika kufanya maamuzi ili nisisusiwe.

Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya mtandao).