Ticker

6/recent/ticker-posts

Tambua na kuepuka mazingira hatarishi (video na maandishi)

TAMBUA NA KUEPUKA MAZINGIRA HATARISHI (Bofya hapa uangalie video)

TAMBUA NA KUEPUKA MAZINGIRA HATARISHI

Maono: Nimeona mtu ambaye alidhani mahali fulani ni salama ni kumbe ni mahali hatarishi sana kwa maisha na uhai wake.

1. Usijifariji wakati moyo unakusuta

Mit 16:25 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

2. Usiruhusu uovu ndani yako

2 Tim 3:12-14 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao.

3. Usitafute ishara na maajabu (acha ishara zikutafute)

Mk 13:21-23 “Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.

Mk 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya.”

4. Epuka vishawishi

Mit 7:1-5, 7-8, 10, 25-27

(i). Tunza Neno la Mungu moyoni na sio akilini

Mst 1-5: “1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.

 2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. 3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. 4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. 5 Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.”

Zaburi 119:11 “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

(ii). Epuka mazingira hatarishi

Mst  7-8: “7 Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, 8 Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake.”

(iii). Epuka watu hatarishi

Mst 10, 25-27: “10 Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; 25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.  26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.  27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.”

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba uondoe uovu ndani yangu ili nisijifariji wakati najua mwisho wangu sio mzuri.

2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kukungoja wewe ili nisidanganywe kupitia miujiza ya uongo

3. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuwa na mikakati ya kushinda vishawishi badala ya kumsingizia shetani kwa kila tatizo linalonipata

Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya mtandao).

Download na kuinstall App ambayo iko kwenye Blog hii. Itakurahisishia kuingia na kujifunza mara kwa mara.