Ticker

6/recent/ticker-posts

PITIA HATUA ZOTE ZA UKUAJI WAKO ULIZOPANGIWA NA MUNGU (Video na Maandishi)

PITIA HATUA ZOTE ZA UKUAJI WAKO ULIZOPANGIWA NA MUNGU (Bofya hapa uangalie video)

PITIA HATUA ZOTE ZA UKUAJI WAKO ULIZOPANGIWA NA MUNGU

Mtoto akipata lishe bora anaweza kukua kwa haraka lakini kamwe hawezi kuruka hatua mojawapo. Mfano huwezi kumkuta mtoto ameota meno yote kwa siku moja.

Ukijaribu kuruka hatua fulani hutakuwa na matokeo mazuri, utapata madhara na hutakuwa na mguso uliokusudiwa. Utafanana na embe lililochumwa kabla ya wakati likalazimishwa kuiva. Haliwezi kuwa na ladha nzuri.

1. Imani hata imani

Warumi 1:17 “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.”

Uwe na imani inayokua. Imani ndogo inafanya mambo madogo:

Marko 4:31,32 “Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi, lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.”

2. Utukufu hata utukufu

2 Kor 3:18 “Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.”

Kutukuzwa ni hatua ya juu ya wokovu wetu.

Warumi 8:30 “Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”

Yn 13:31,32 “Basi huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.”

 3. Nguvu hata nguvu

Zaburi 84:5-7 “Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka. Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.”                              

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba imani yangu ikue ili niweze kupokea mambo makubwa na kufanya mambo makubwa kwa Jina Lako.

2. Ee Mungu naomba niwe na wokovu wenye utukufu wa Mungu na sio kujitukuza mwenyewe.

3. Ee Mungu naomba niwe na nguvu inayobadilisha bonde la vilio kuwa chemchemi za baraka.