Ticker

6/recent/ticker-posts

Wokovu ni zaidi ya sala ya toba (Video na Maandishi)

WOKOVU WA KWELI NI ZAIDI YA SALA YA TOBA (Bofya hapa uangalie video)

WOKOVU WA KWELI NI ZAIDI YA SALA YA TOBA

Ndoto: Nimeona watu wengi wakichoka kusubiri na kuamua kuondoka kabla ya kupokea kile walichokuwa wameitiwa. Wengine walipoona wenzao wanaondoka waliwafuata bila hata kujiuliza kwanini wanafanya hivyo.

Ebr 2:3 “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.”

Maeneo ambayo tunahitaji kuokolewa

1. Kuokolewa na dhambi: Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.”

2. Kuokolewa na dunia hii mbovu: Wagalatia 1:4 “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.”

3. Kuokolewa na ghadhabu itakayokuja: 1 Wathesalonike 1:10 “na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.”

Tito ameeleza kwa muhtasari: Tito 2:11-14 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;  tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.”

 

Tufanyeje ili tuwe salama?

 

1. Tuvumilie hata mwisho

Mathayo 10:22 “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”

Yakobo 5:11 “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”

2. Baada ya kuokolewa tunatakiwa KUSHINDA na sio kubweteka

Ufunuo wa Yohana 3:4,5 “Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.”

Achana na imani potofu kwamba ONCE SAVED, ALWAYS SAVED.

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba unisaidie nishinde dhambi badala ya kujifariji na sala ya toba wakati sina matendo mema.

2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuvumilia hata mwisho nisije nikakosa uliyoniandalia kwa kuchoka kusubiri.

Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya mtandao).