ROHO YA KUTANGA-TANGA HAITAKUTESA TENA (Bofya hapa uangalie video)
ROHO
YA KUTANGA-TANGA HAITAKUTESA TENA
Ndoto: Hivi karibuni niliona nikiwaombea watu kwamba roho
ya kutangatanga iwaachie.
1. Katika
kuabudu kwako
Mungu anakwenda kukutoa kwa wachungaji waliokufanya chakula
chao
Ezekieli 34:6,10 “Kondoo zangu walitanga-tanga katika
milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu
ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.
Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo
zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao
wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo zangu vinywani
mwao, wasiwe tena chakula chao.”
2.
Katika kufikiri kwako
2 Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana
na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika
akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.”
3. Katika kazi zako
Mungu anakwenda kuondoa laana ya kutanga-tanga ndani yako – hata ukihama miji, sehemu za kazi na kubadili biashara hufanikiwi
Mwanzo 4:12 “utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.”
Sasa ufanyeje?
1. Unatakiwa kujihoji na kumrudia Mungu – tunasikiliza zaidi utabiri wa hali ya hewa kuliko manabii wa Bwana.
Amosi 4:7,8 “Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika. Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.”
2. Usilitaje bure Jina la Yesu ambaye huna uhusiano naye
Matendo ya Mitume 19:13,15,16 “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.”
3.
Omba upewe roho iliyotulia (steadfast spirit) – roho ya kuwa na
msimamo katika kusudi bila kuyumbayumba – uwe reliable, dependable.
Zaburi 51:10 “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani
yangu.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba uondoe ndani yangu roho ya kutangatanga
kiroho, kiakili na kimaisha.
2. Ee Mungu naomba unipe moyo safi na roho iliyotulia ndani
yangu.