Nashukuru uongozi wa shule ambao umeona umuhimu wa kunialika
kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na kushinda unyanyasaji wa
kingono ambao umekithiri mashuleni.
Tuko katika kipindi ambacho wanafunzi wako katika uhatarishi
mkubwa kwa sababu mkazo mkubwa ni katika ufaulu wa masomo ya kitaaluma tu bila
kuwasaidia wanafunzi wajitambue na kupata stadi za maisha za kukabiliana na
changamoto za maisha. KUNA MAKATAZO MENGI LAKINI HAKUNA MBINU ZA KURAHISISHA
UTEKELEZAJI WAKE!
Kadiri Mungu atakavyotujalia hatutaishia kwa wanafunzi bali tutawafikia
pia walimu, wazazi na viongozi wa dini. Wazazi tunakagua zaidi madaftari lakini
hatukagui maeneo mengine ya maisha ya watoto wetu. Mpaka tukiona mtoto anachechemea
ndipo tunafuatilia na mara nyingi tunakuwa tumeshachelewa sana. Tunapenda kuwasaidia
watoto na wazazi wavunje ukimya na kuweza kujadili kuhusu afya ya uzazi na
watoto wao bila aibu. Mtoto asipoweza kutuuliza sisi kama chanzo sahihi cha
taarifa, atauliza marafiki zake na mitandao ya kijamii na kukutana na
upotoshaji.
Ombea na kuwezesha huduma hii kadiri unavyojaliwa ili
tukinusuru kizazi chetu na majanga yanayoepukika.
Dr Lawi Mshana, 0712-924234