KARIBU USHIRIKI BARAKA ZA KWENDA KUWATIA MOYO WATUMISHI NA VIONGOZI WA BURUNDI NA DRC CONGO
Neno la Mungu linasema kwamba Roho wa Mungu akitujilia
tutapata uwezesho wa kuwa tayari kujikana, kujinyima na hata kufa ili tuwafikie
walio karibu na walio mbali nasi. Mdo
1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu
yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika
Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Je nguvu hii ya Roho Mtakatifu ilikusudiwa itumike tu kwenye
maombi na mikutano katika maeneo tunayoishi hadi kufa kwetu? Jibu ni hapana.
Bilashaka baadhi yenu mliungana nami wakati nilipopeleka neno
la Mungu Malawi na Zambia. Sasa nimepata mwaliko wa kwenda Burundi na DRC Congo
kufanya semina za kujengea uwezo viongozi kutoka madhehebu mbalimbali.
Naomba uungane nami kwa sadaka yako ya upendo ya TZS elfu 5
(USD 2) au zaidi ili tugawane thawabu hii ya kuwafikia wengine na kutimiza
Agizo Kuu tulilopewa na Bwana. Warumi 10:15 “Tena wahubirije, wasipopelekwa?
Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”
Natarajia kwenda kufanya huduma hiyo mwezi Mei 2024.
Mungu akukumbuke kwa kushiriki uwekezaji huu katika ufalme
wa Mungu ambapo hakuna hasara na ambapo ni benki ya akiba utakayoikuta baada ya
maisha haya.
Mathayo 6:19,20 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi.”
Unaweza kutuma kwenye simu yangu Lawi Mshana, 0712-924234
au akaunti namba 0152219784300 (CRDB Bank). Naomba ukituma unijulishe ili
nizidi kukuweka mikononi mwa Mungu.
Karibu sana!