POKEA UTAMBULISHO MPYA (Bofya hapa kuangalia video)
POKEA
UTAMBULISHO MPYA
Utangulizi: Nimepata maono ya kuomba na wewe maeneo
mbalimbali ambayo unapata changamoto. Leoa tutaombea utambulisho wako.
1 Nya 4:9,10 “Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”
Muombe Mungu akusaidie ili jina baya ulilopewa lisiwe legacy yako (urithi) au destiny (hatima) yako.
Isaya 62:2 “Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Nakataa majina mabaya niliyopewa na
ndugu na jamii ambayo yanaathiri hatima ya maisha yangu katika Jina la Yesu.
2. Ee Bwana
naomba unipe jina jipya na utambulisho
mpya ambao utazika historia mbaya ya maisha yangu ya nyuma katika Jina la
Yesu. Rudisha utambulisho ulioibiwa!
3. Naomba utambulisho wa kazi zangu ubebe uwepo wa Mungu na kuvuta upendeleo wa wateja watarajiwa
na mikataba mipya katika Jina la Yesu.
4. Ee Bwana nipe mawazo ya kiubunifu kwa ajili ya
kutosheleza wateja wangu na wafadhili wangu katika Jina la Yesu.
KWA USHAURI NA MAOMBI UNAWEZA KUWASILIANA NAMI KWA SIMU
NAMBA 0712-924234

