USIONE AIBU KUMFICHUA SHETANI ANAVYOKUTESA (Bofya hapa uangalie video)
USIONE
AIBU KUMFICHUA SHETANI ANAVYOKUTESA
Utangulizi: Shetani ana mbinu nyingi za kutesa watu. Kuna
watu amewapa aibu waogope kuweka wazi matatizo yao ili shetani aendelee
kuwakandamiza. Unapoona aibu kumwambia daktari tatizo lako unaliongeza zaidi au
kukosa ufumbuzi wa kudumu.
Kilichomleta Yesu duniani ni kuharibu kazi za ibilisi. 1
Yohana 3:8 “atendaye dhambi ni wa
Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa
Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.”
Mtume
Paulo hakuficha tatizo alilopata kutokana na shetani
1 Wathesalonike 2:18 “Kwa
hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na
Shetani akatuzuia.”
Hatumshindi shetani kwa kwenda kichwakichwa. 2 Wakorintho 2:11 “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira
zake.”
2 Wakorintho 12:7 “Na
makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa
mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita
kiasi.”
Yesu alipojaribiwa nyikani, alimkemea shetani kwa kumpa sababu (kujibu hoja yake). Mt 4:9-11 “akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Natangaza kila eneo la maisha yangu linalotawaliwa na shetani liachiliwe huru
katika Jina la Yesu.
2. Napokea ukombozi kamili kutoka
katika aibu ya kugonga milango na kubip
na kupiga simu mara kwa mara za kuomba msaada wa kifedha katika Jina la
Yesu.
3. Ee Bwana nifungue kutoka katika
taabu ya kazi zisizo na faida na
shughuli zinazochanganya kichwa changu katika Jina la Yesu.
4. Ee Mungu naomba unilinde dhidi ya
udanganyifu wa kunitapeli
nilichotaabikia katika Jina la Yesu.