Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII INAHITAJI WAWEZESHAJI MAKINI ILI ISHINDE CHANGAMOTO




JAMII INAHITAJI WAWEZESHAJI MAKINI ILI ISHINDE CHANGAMOTO

Leo tumekuwa na warsha ya kujengea uwezo wawezeshaji kwa ajili ya marika mbalimbali katika jamii ikiwa ni pamoja na wanafunzi. Mpango huu unalenga pia kuwafikia walezi wakuu wa watoto ambao mara nyingi wanasahaulika kwamba nao pia wanakutana na changamoto zinazowakatisha tamaa. Walezi hao ni wazazi/walezi, walimu, wahudumu wa afya na viongozi wa dini.

Baadhi ya watumishi wa jamii wana maumivu yaliyovia ndani ya mioyo yao ambayo kama hayakushughulikiwa yanawafanya wawe wachungu kwa watu wanaowahudumia. Kwa vile nao ni binadamu hatupaswi kuwanyoshea kidole bila kuwa na mkakati wa kuwajengea uwezo ili waweze kukabiliana na changamoto zao kwa ushindi. Watumishi wengi wanaonyanyasa watu walipitia magumu fulani katika historia ya maisha yao hivyo ni kama wanaolipiza kisasi katika jamii.

Wawezeshaji wamejifunza njia bora za kuwezesha watoto na watu wazima na mambo ya kuepuka wanapofanya kazi na watoto ili kuhakikisha wanakuwa salama. Jamii haibadiliki kwa kupewa tu mafunzo (training) bali kwa kuhakikisha inajengewa uwezo (empowerment).

Wasiliana nasi ili huduma hii ikufikie kupitia mpango wetu wa Nitatoboa Initiative.

Dr Lawi Mshana, Beyond Four Walls, 0712-924234