BARIKIWA KWA KUWASAIDIA WATU WASIOWEZA KUKULIPA
Tunashukuru sana kwa zawadi ya nguo kutoka kwenye familia
ya Muheza, Tanga kwa ajili ya watu wanaoishi mazingira hatarishi wanaopokea misaada
kupitia kwetu. Tuzidi kuwa na utamaduni wa kusaidia wasiojiweza badala ya kuwaachia
watu wagombanie masanduku yetu ya nguo baada kuondoka kwetu duniani. Kuna mtu
anahitaji sana vitu vyako ambavyo kwa sasa huvitumii.
Unaposaidia watu ambao pengine hawastahili upendo wako na
hakuna hata siku moja watakushukuru kwa vile hawakujui, utapata thawabu kubwa
mbinguni.
Luka 6:35 “Bali
wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu
yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema
kwa wasiomshukuru, na waovu.”
Karibu sana uungane nasi katika utumishi huu
usio na mipaka ya kidini wala kiitikadi.
Tunapokea misaada hii kutoka mahali popote
ulipo.
Dr. Lawi Mshana, 0712-924234 (Simu na
Whatsapp)