Ticker

6/recent/ticker-posts

Mpe Mungu sababu ya kukubariki (kaa mkao wa kubarikiwa)

Mpe Mungu sababu ya kukubariki (video)

Mpe Mungu sababu ya kukubariki (kaa mkao wa kubarikiwa)

Hivi karibuni nikiwa safarini nilisikia sauti ndani ya moyo wangu ikisema, “MPE MUNGU SABABU YA KUKUBARIKI.” Ilibidi niandike maneno haya.

Mungu yuko tayari wakati wote kutubariki. Na sisi tunahitaji sana kupata baraka kutoka kwake.

Maswali ya kujiuliza ni:

1. Je, tunaweza kumpa Mungu sababu ya kutubariki?

2. Tuna sifa za kupokea baraka zake?

3. Mungu ananufaika na baraka tunazomuomba?

Ingawa mara nyingi tunahita msaada wa Mungu. Hata Yeye kuna kitu anahitaji kutoka kwetu?

1. Anataka umche, utende mapenzi yake, umpende na kumtumikia

Kum10:12 “Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.”

2. Anataka utende haki (usidhulumu watu), upende rehema na kuwa mnyenyekevu

Mika 6:8 “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”

3. Anataka ujali kujitakasa, usijiinue na usiape kwa hila

Zab 24:3-5 “3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? 4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. 5 Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.”

Baraka kutoka kwa Mungu zinahitaji KUKAA MKAO WA KUBARIKIWA kuliko KUFUNGA NA KUOMBA ILI TUBARIKIWE. Yaani, kuwa sumaku ya kuvuta baraka Zake.

Kumbuka ni Yeye Mwenyewe amesema anataka tubarikiwe na sio sisi tulioanzisha kwa maombi yetu.

Jambo muhimu katika ‘kukaa mkao wa kubarikiwa na Mungu’ ni KUTII MAAGIZO YAKE.

Unaweza kuhoji kwamba, ‘Mbona wengi wasiomtii wala kumjua Mungu wamebarikiwa?’ Kumbuka baraka sio KUMILIKI PEKE YAKE BALI NI KUFURAHIA UNACHOKIMILIKI. Shetani anaweza kumpa mtu pesa nyingi lakini KAMWE HATARUHUSU MTU HUYO AZIFURAHIE. Atakuwa anajionyesha tu kwa watu ili awe mtego wa kuwanasa waingie, lakini anapewa masharti magumu sana kama vile kutoruhusiwa kuoa, kutoruhusiwa kuvaa vizuri, kutoruhusiwa kulala ndani ya nyumba bali nje kwenye gari, kutembea makaburini usiku wa manane, kumtoa mtu anayempenda atolewe kafara, kuruhusiwa kuishi duniani kwa miaka michache na kisha kufanywa msukule nk

Huwezi kupokea baraka za Mungu kama ni muumini vuguvugu. Wapo pia tunaodhani wamebarikiwa na Mungu lakini sivyo. Wamepata mali kwa kuhonga, kugushi, kuiba, kudhulumu, kutembea na bosi wako nk

Je Mungu anataka tuishi maisha ya baraka duniani au mpaka tukifika mbinguni?

1. Mungu anataka tule mema ya nchi kwa masharti ya KUMTII

Isaya 1:19 “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi.”

2. Mungu anataka baraka zake zitupate (zitu-overtake) kwa KUTII MAAGIZO YAKE

Kum 28:1,2 “1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.” Andiko hili linasema BARAKA ZA MUNGU ZITAKU-OVERTAKE KAMA UTASIKIA SAUTI YA MUNGU!

Mungu akutane na haja ya moyo wako!

Dr. Lawi Mshana, +255712-924234 (sms au whatsapp), Korogwe, Tanga, Tanzania