Yesu anataka kukuvusha, usiogope! (video) – Mama Mchungaji Lawi
Yesu anataka kukuvusha, usiogope!
(video) – Mama Mchungaji Lawi
Yesu
aliyemshika Petro asizame na akatuliza mawimbi ya bahari, yuko tayari
kukusaidia hata wewe leo.
Unachotakiwa
tu – usisahau kumuita ili ‘akuokoe.’
Mt 14:28-32 “28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. 31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? 32 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.”
Mambo ya kujifunza hapa:
1. Penda kujaribu mambo ambayo hujawahi kuyafanya – Petro
hakuridhika kumuangali tu Yesu akitembea juu ya maji. Alitamani na yeye pia
kupata uzoefu huo na akachukua hatua ya kuomba apewe uwezo huo.
2. Petro aliweza kutembea juu ya maji kama Bwana Yesu aliposikia
sauti ya Bwana na kuchukua hatua - Hakikisha unasikia sauti ya Mungu ya kukupa
kibali kabla kuchukua hatua. Usijiaminishe mwenyewe.
3. Petro alipotazama UPEPO badala ya BWANA YESU alizama -
Ukitoa macho yako kwa Mungu na kuangalia majaribu yako lazima utazama.
4. Petro hakusahau kwamba aliyemuwezesha ni Bwana Yesu.
Hivyo alimuita ili amuokoe – Usisahau kwamba Bwana yuko karibu sana na wewe
hata kama unapitia magumu. Anasubiri upaze sauti yako na kumuita.
5. Bwana Yesu alimshika Petro mkono alipohitaji msaada Wake – Mungu anasubiri utamke mwenyewe kwamba unahitaji msaada wake au wokovu wake.
Pata ujumbe huu kwa wimbo wa Injili alioimba Minja Mshana.
Dr. Lawi Mshana, +255712-924234 (sms au whatsapp), Korogwe, Tanga,
Tanzania