Ticker

6/recent/ticker-posts

MUNGU ANAZIDI KUGUSA WATANZANIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA HUDUMA YETU KWA AJILI YA JAMII


MUNGU ANAZIDI KUGUSA WATANZANIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA HUDUMA YETU KWA AJILI YA JAMII

Tunashukuru kwa kupokea tena sadaka ya upendo kutoka kwa mdau wa maendeleo kutoka Singida. Mungu hatamsahau kwa huu moyo wake wa utoaji. Naomba Mungu atatimiza ndoto alizo nazo kwa wakati.

Naamini kwamba kama Watanzania tutaamua, tunaweza kusaidia wasiojiweza na wanaoishi mazingira hatarishi na kuepuka misaada yenye agenda mbaya kutoka kwa wasiotutakia mema. Tuna vitu vingi vyenye thamani ambavyo tumevilundika tu nyumbani au ofisini kwa vile kwa sasa tumepata vipya.

Dhima ya shirika letu ni kujenga uwezo wa jamii ishinde uhatarishi, umasikini na utegemezi kwa kutumia MBINU SHIRIKISHI. Kwa lugha nyingine ni kutumia uwezo tulio nao kuliko kutegemea wafadhili kwa kila kitu. Kuwa tegemezi wa wafadhili kwa kila kitu kunawafanya watupangie maisha yetu na kuchukua uhuru wetu.

Karibu sana uwe sehemu ya wito huu mkuu kwa ajili ya taifa letu bila ubaguzi wa kidini, kijinsia, kikabila na kimatabaka.

Wasiliana nasi wakati wowote. 0712924234 (simu au Whatsapp)

Dkt. Lawi Mshana, Beyond Four Walls (Ofisi zetu: Korogwe Mji & Ihumwa, Dodoma Jiji)