TUMETUMWA KUHUBIRI DINI AU UFALME? (video)
TUMETUMWA
KUHUBIRI DINI AU UFALME?
Ukifuatilia vizuri maandiko utagundua kwamba Bwana Yesu
na mtangulizi wake, Yohana Mbatizaji walihubiri kuhusu ujio wa Ufalme wa Mungu
duniani na namna ya kujiandaa kuupokea.
Mathayo 4:17 “Tokea wakati
huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni
umekaribia.” Luka 4:43 “Akawaambia,
Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia;
maana kwa sababu hiyo nalitumwa.”
Hata sisi tumeagizwa kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na sio kuwa
watu wa dini, ndipo tutazidishiwa.
Mathayo 6:33 “Bali
utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
1. Bwana Yesu alipinga sana mitazamo ya kidini ya kipindi chake –
inawafungia watu washindwe kuingia katika Ufalme
Mathayo 23:13 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo,
wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe
hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.”
2. Dini ilihusika sana katika kuzuia mpango wa Yesu duniani – walibeza huduma ya Yesu ya kuleta wokovu
(viongozi wa dini waliishinikiza Yesu auawe wakati serikali ilitaka kumuachia
huru)
Luka 23:4 “Pilato
akawaambia wakuu wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo ovu katika mtu
huyu.”
Mathayo 27:20 “Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.”
Mathayo 27:41 “Kadhalika
na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema,
Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.”
3. Somo la Bwana Yesu la jinsi ya kuomba limeanza na maombi ya
UTAWALA WA MUNGU UREJESHWE DUNIANI (tuishi
duniani kama mbinguni)
Lk 11:2,3 “Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe siku kwa siku riziki yetu.”
4. Mwisho unachelewa kwa sababu tunahubiri dini kuliko Ufalme wa
Mungu
Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa
katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho
utakapokuja.”
5. Kuna dini safi na chafu
Yakobo 1:27 “Dini
iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima
na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”
Mungu atupe ufunuo kuhusu ufalme wa Mungu ulivyo tofauti na dini ili tutawale mazingira yetu, na mwishowe twende mbinguni.
Dr. Lawi Mshana, +255712-924234 (sms au
whatsapp), Korogwe, Tanga, Tanzania

