TULIMALIZA
SALAMA HUDUMA YA BURUNDI. NIKAGUNDUA KWANINI MUNGU ALINIPA FURSA YA KUSOMA
LUGHA YA KIFARASA MIAKA ILIYOPITA.
Namshukuru sana Mungu kwa namna alivyoonekana
kipekee katika huduma ya Burundi. Watu waliweke pembeni tofauti zao za kimadhehebu.
Lakini pia nilifurahia sana ukarimu wa Warundi. Kila kanisa wamama wanakuwa na
huduma ya kipekee sana. Hawakumsahau mke wangu hivyo walinikabidhi zawadi yake
wakitambua kwamba huduma hii haingefika popote bila usaidizi wake.
Nilikutana na watu wengi ambao hawajui Kiswahili
wala Kingereza isipokuwa wanajua Kirundi na Kifaransa. Hivyo sikupata shida kwa
vile nilisoma hii lugha kwa miaka minne hapa kwetu Tanzania ingawa ni miaka
mingi iliyopita. Nimegundua kwa nini nimekuwa nikipokea mialiko kutoka nchi
zinazozungumza Kifaransa. Mungu anataka kutumia kila alichotujalia kuwa nacho
kwa utukufu Wake.
Nawashukuru wote mliohusika katika umisheni huu.
Naomba usichoke kutenda mema kwani utavuna kwa wakati wake. Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana
tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.”
Kama tulivyokusudia kuzifikia nchi mbalimbali
tukianzia na hizi tunazopakana nazo, nimeona Mungu akifungua milango. Alikuwepo
mchungaji kutoka Uganda. Naye ameomba huduma hii iwafikie waumini na wachungaji
wa huko.
Tutakaposhirikishana kuchangia huduma hiyo naomba
tuitikie tena kwa vile tunajiwekea akiba mbinguni kusiko na wezi wala kutu. Kumbuka
vitu vingi tulivyo navyo hapa duniani, siku tukiondoka wengine watagawana na tutasahaulika.
Mathayo 6:20 “bali jiwekeeni hazina
mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala
hawaibi.”
Neema ya Mungu iwe nawe daima.
Dr. Lawi Mshana, Korogwe, Tanga, Tanzania;
+255712924234





