UKITAKA KUPATA THAWABU SAIDIA WATU WASIOWEZA KUKULIPA
Ni rahisi sana kwa wengi kuchangia sherehe
na misiba kwa vile unajua kuna siku utahitaji pia kuchangiwa (malipo ya
kibinadamu). Lakini kama unataka kupata thawabu kwa Mungu unatakiwa kufanya
kinyume chake.
Lk 14:12-14 " 12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije
wakakualika wewe ukapata malipo. 13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, 14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki."
Tumepokea tena sadaka ya upendo ya nguo kutoka Morogoro kwa ajili ya huduma tunazotoa kwa jamii. Walengwa wetu wakuu ni watu wanaoishi mazingira hatarishi na waathirika wa ukatili ambao wamethibitika kuwa katika hali hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya serikali na jamii. Hatuwatambui
sisi wenyewe bali tunashirikiana na wadau kuhakiki uhatarishi wao.
Shirika letu la Beyond Four Walls linalenga kuihamasisha jamii yetu iunge mkono juhudi za kusaidia jamii. Hata sisi tunaweza kutoa mitumba na sio mpaka itoke nje ya nchi.
Angalia pia kwako inawezekana una kitu ambacho kinatufaa katika ofisi yetu ambacho hukitumii kwa sasa. Tunakukaribisha sana. Mfano, kompyuta, fanicha, nguo (za kuvaa, mashuka, viatu), vyombo vya
usafiri nk.
Karibu sana na Mungu akubariki kwa moyo wako wa utoaji.
Beyond Four Walls, Korogwe, Tanga, Tanzania; +255712-924234 au +255657705509