Ticker

6/recent/ticker-posts

Kanuni za mafanikio Na 3: Kutoa raslimali zako kwa kuzingatia msimu


Kanuni ya mafanikio Na 3: Kutoa raslimali zako kwa kuzingatia msimu

Video: Na 3: Kutoa raslimali zako kwa kuzingatia msimu

Baada ya kutoa zaka unatakiwa kutoa sadaka kutokana na asilimia 90 (90%) uliyobaki nayo. Kimsingi zaka sio ya kwako. Hivyo usipotoa zaka umeiba. Utoaji wako uko katika asilimia 90 uliyobaki nayo. Unaweza kupanda mbegu kwa kutumia kiasi cha kwako na sio kupitia zaka.

Lakini pia lazima utambue kwamba hata mkulima hawezi kufanikiwa kwa kupanda mbegu peke yake. Lazima atambue msimu mzuri wa kupanda. Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna. hii ina maana kwamba kuna wakati Mungu anakupa MKATE ili ufurahie upandaji wako wa siku zilizopita na MBEGU ili upande kwa ajili ya siku zijazo. 2 Wakorintho 9:10 "Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu."

Mhubiri 3:2 "..... Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa."

Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania