Video: Na 4: Kutoa kwa wingi ukiwa unafurahia moyoni
Kanuni za mafanikio Na 4: Kutoa kwa wingi ukiwa unafurahia moyoni
(usilazimishwe na mtu)
Kumekuwa na tabia ya waumini kulazimishwa na kupangiwa kiasi cha kutoa. Huo sio mpango wa Mungu.
Mungu anataka utoe sadaka kwa moyo wa kupenda na sio kwa kulazimishwa. 2 Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
Kutoka 25:2 "Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu."
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania