KUSHINDA UBAHILI (JIFUNZE KUMKOPESHA MUNGU)
Mit 11:24,24 “24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. 25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.”
Unapowabariki watu unaongezewa zaidi kuliko ukiweka akiba peke yake. Kuweka akiba kunasaidia maisha yako ya baadaye kwa JINSI YA MWILI (benki ya duniani) na kubariki watu kunasaidia maisha yako ya baadaye kwa JINSI YA ROHONI (unakuwa umeweka akiba katika benki ya mbinguni).
Mit 19:17 “Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.”
Kumsaidia maskini ni kuweka akiba kwa Mungu ili siku moja akukumbuke (ni sawa na kumkopesha Mungu).
Zab 41:1 “Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.”
Ukiwakumbuka maskini na wahitaji kuna siku Bwana atakusaidia ukipitia wakati mgumu. Kusaidia maskini ni kuweka akiba kwa Mungu maana umekubali kuwa mkono Wake kwa ajili ya kugusa wahitaji.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator
& Public Speaker, +255712924234, Tanzania