Video link: Mtu wa Mungu anabarikiwa ili awe mfereji
21. A man of God is blessed to be a channel
(Mtu wa Mungu anabarikiwa ili awe mfereji)
God blesses us to BLESS OTHERS and not just for achieving our selfish goals. We see wealthy people today who do not care about the poor around them. The Bible teaches us that success from God is not like that of this world. The worldly success is selfish because it doesn't care about teaching others the principles of a successful life. Gen 12:2 “I will make you a great nation; I will bless you and make your name great; And you shall be a blessing.” We learn that God can lift us and give us great success, but not for ourselves. God wants you to be His hand or channel for touching people with various needs. Satan is happy to see you continue to be rich while others are suffering, and he makes sure that you do not enjoy the wealth you have. God's goal to bless you is for you to be a blessing. God did not give you the blessings you have for yourself. Someone needs to share those blessings, too.
Please send your love gift to support this ministry (Tafadhali tuma sadaka yako ya upendo kuendeleza huduma hii). +255 712924234 or CRDB Bank; Account Name: Lawi E. Mshana; Account Number: 0152219784300; Swift Code: CORUTZTZ
Mungu anatubariki ili TUWABARIKI WENGINE na sio tu kwa ajili ya kufikia malengo yetu ya kichoyo. Wako matajiri leo wanaomiliki mali nyingi sana lakini hawajali masikini wanaowazunguka. Biblia inatufundisha kwamba mafanikio kutoka kwa Mungu sio kama ya dunia hii. Mafanikio ya dunia ni ya kujijali mwenyewe bila kuwafundisha wengine mbinu ya mafanikio. Mwa 12:2 “nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka.” Tunajifunza kwamba Mungu anaweza kutuinua na kutupa mafanikio makubwa lakini sio kwa ajili yetu wenyewe. Mungu anataka uwe mkono wake au mfereji wake kwa ajili ya kuwagusa watu wenye mahitaji mbalimbali. Shetani anafurahi kuona unaendelea kuwa tajiri wakati wengine wakiteseka na wewe mwenyewe akikupa masharti magumu yanayokufanya usifurahie utajiri ulio nao. Lengo la Mungu kukubariki ni wewe uwe baraka. Mungu hakukupa baraka ulizo nazo kwa ajili yako mwenyewe. Kuna mtu fulani anatakiwa kushiriki baraka hizo pia.
Bofya video usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator & Trainer, +255712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)