Ticker

6/recent/ticker-posts

Empowering students to achieve their dreams (Kujengea uwezo wanafunzi watimize ndoto zao)

Video link: Kujengea uwezo wanafunzi

Empowering students to achieve their dreams (Kujengea uwezo wanafunzi watimize ndoto zao)

We need to excel academically and prosper in life. It is essential to study and pass our exams until we reach higher education and college. However, try not to bury your talent. Develop your talent as it can make you successful in your life. There are people today who go around offices with certificates to apply for jobs. They forget that they have skills and experience that can give them a breakthrough in their lives. You need to realize who you are. You have something unique that only you can do. Along with your studies, you must realize who you want to be in the future. If you do not know who you want to be, you will be determined by the education system instead of achieving your dreams. You may find yourself studying for things that are wasting your time.

Kujengea uwezo wanafunzi watimize ndoto zao

Tunatakiwa kufaulu shule na kufaulu maisha. Ni muhimu sana kusoma na kufaulu mitihani yetu mpaka tufike elimu ya juu na chuo. Hata hivyo ujitahidi usizike kipaji chako. Kiendeleze kipaji chako kwa vile kinaweza kukufanikisha katika maisha yako. Kuna watu leo wanazunguka maofisini na cheti ili kuomba kazi. Wanasahau kwamba wana ujuzi na uzoefu unaoweza kuwapa upenyo katika maisha yao. Unatakiwa kujitambua kwamba wewe ni nani. Una kitu cha kipekee ambacho ni wewe tu unakiweza. Pamoja na kusoma kwako lazima utambue kwamba unataka kuwa nani baadaye. Usipojua kwamba unataka kuwa nani, utapangiwa na mifumo ya elimu badala ya kufikia ndoto zako. Unaweza kujikuta unasomea vitu ambavyo unapoteza muda wako bure.

Dr Lawi Mshana, Facilitator, +255712924234, Tanzania