No. 14. The finished work of Christ (Kazi aliyomaliza Kristo msalabani) – Online Conference
Living in the fullness of Christ's work. There are people who, although they are saved, still remember their old lives. You can find a person praising his success before being saved because he has not yet recognized the beauty of Jesus, who saved him. This kind of person has not realized what he has received through the cross of Jesus. 2 Cor 5:17 “Therefore, if anyone is in Christ, he has become a new creation; old things have passed away; behold, all things have become new.” Some people misinterpret this scripture. They think that if a person is saved, he no longer needs a ministry of deliverance simply because he repeated the prayer of repentance. This scripture means that when you are saved, you begin a new life - a new journey of your deliverance. Positive life changes must occur after believing in Jesus. We should not be more concerned with the deliverance of others spiritually and forget to pray for ourselves. Our Christianity should not only be seen in worship services but also in our homes. We must remember that we are to tear down the altars of the devil and build the altars of God. However, God's altar is not only built in the church building but also in our homes.
Kazi aliyomaliza Kristo msalabani
Kuishi katika utimilifu wa kazi ya Kristo. Kuna watu ingawa wameokoka, bado wanakumbuka maisha yao ya kale. Mtu mwingine anasifia mafanikio yake kabla ya kuokoka kwa vile bado hajaona uzuri wa Yesu aliyempokea. Mtu wa aina hii hajatambua alichopokea kupitia msalaba wa Yesu. 2 Kor 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” Kuna watu wanalitafsiri vibaya hili andiko. Wanadhani mtu akiokoka hahitaji tena huduma ya kufunguliwa au ukombozi kwa vile tu ameongozwa sala ya toba. Andiko hilo linamaanisha kwamba ukiokoka unaanza maisha mapya – safari mpya ya ukombozi wako. Lazima mabadiliko chanya ya maisha yatokee baada ya kumwamini Yesu. Tusitumie nguvu kubwa kuwafungua wengine kiroho na kusahau kujiombea sisi wenyewe. Ukristo wetu usionekane tu ibadani bali hata nyumbani kwetu pia. Tukumbuke kwamba tunatakiwa kubomoa madhabahu za shetani pamoja na kujenga madhabahu ya Mungu. Hata hivyo madhabahu ya Mungu haipo kanisani tu bali pia katika nyumba zetu.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania