No. 6. The finished work of Christ (Kazi aliyomaliza Kristo msalabani) – Online Conference
We have many Bible concepts that we know, but they don't come to fruition. Remember that if the first Adam had not sinned, we would not have to go to Heaven but would have lived on earth in peace forever. After Jesus came to earth and upgraded us, He had to prepare a place for us in Heaven. We had no place in heaven. We have been given a rare opportunity that only a few people will manage to take. Even the scriptures tell us that few will be able to enter through the narrow door. Luke 13:24 “Strive to enter through the narrow door, for many, I tell you, will seek to enter and will not be able.” Our bodies do not desire to go to Heaven, but our spirits desire to go to Heaven. We need the help of the Holy Spirit to overcome sin. Jesus overcame because He was led by the Spirit. We also need to overcome the words of the devil by using the Word of God. We must know how to protect and defend our faith.
Kazi aliyomaliza Kristo msalabani
Tuna dhana nyingi za Biblia tunazozijua lakini haziwi kitu halisi. Kumbuka kama Adamu wa kwanza hangetenda dhambi hatungeenda mbinguni bali tungeishi duniani kwa raha milele. Baada ya Yesu kuja duniani na kutupandisha daraja ili tuende mbinguni, imebidi atuandalie makao. Hatukuwa na makao mbinguni. Tumepewa fursa adimu ambayo sio wengi wataweza kufikia viwango hivyo. Hata maandiko yanatuambia kwamba ni wachache watakaoweza kuingia katika mlango mwembamba. Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.” Miili yetu haitamani kwenda mbinguni ila roho zetu zinatamani kwenda mbinguni. Tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu ili tushinde dhambi. Yesu alishinda kwa vile aliongozwa na Roho. Tunahitaji pia kushinda maneno ya shetani kwa kutumia Neno la Mungu. Ni muhimu tujue jinsi ya kuilinda na kuitetea imani yetu.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania