Video link: Na. 9. Kazi aliyomaliza Kristo msalabani
No. 9. The finished work of Christ (Kazi aliyomaliza Kristo msalabani) – Online Conference
Jesus became our Passover. When Jesus was on earth, He celebrated the Jewish Passover until He became the Passover Himself. So we need to change the way we celebrate Passover now. John 11:55 “Now the Passover of the Jews was near, and many went up from the country to Jerusalem before the Passover to purify themselves.” We sin by enjoying ourselves instead of purifying ourselves.
1 Cor 5:7 “Purge out therefore the old leaven, that you may be a new lump, as you are unleavened. For Christ our Passover is sacrificed for us.” Christ Himself is the Lamb of God. Let us make room for Jesus (our Passover) rather than just the Passover day. 1 Peter 1:19 “but with the precious blood of a lamb without blemish or spot, that is, of Christ.” The Lord Jesus fulfilled the requirements of the Lamb without blemish or spot, and was qualified to take away the sins of the world. And He did this only once. We no longer need to slaughter a lamb every year for the forgiveness of our sins.
Kazi aliyomaliza Kristo msalabani
Yesu alifanyika Pasaka yetu. Yesu alipokuwa duniani alisherehekea Pasaka ya Kiyahudi mpaka alipofanyika Pasaka Yeye mwenyewe. Kwa hiyo tunatakiwa kubadilika namna tunavyosherehekea Pasaka kwa sasa. Yn 11:55 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase.” Tunakosea kwa kujifurahisha badala ya kujitakasa.
1 Kor 5:7 “Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.” Kristo Mwenyewe ndiye Mwanakondoo wa Mungu. Kwa hiyo tumpe nafasi Yesu (Pasaka wetu) kuliko siku ya Pasaka. 1 Petro 1:19 “bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” Bwana Yesu alitimiza vigezo vya Mwanakondoo asiye na ila wala waa hivyo akawa na sifa za kubeba dhambi za ulimwengu. Na alifanya hivyo mara moja tu. Hatuhitaji tena kuchinja mwanakondoo kila mwaka kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania