Video link: MWISHO UMEKARIBIA, TUWE NA AKILI
THE END IS NEAR, LET US BE SENSEFUL
(MWISHO UMEKARIBIA, TUWE NA AKILI)
We see that two thousand years since the Lord Jesus came to earth is a long time. In fact, they are only two days to Him.
1 Peter 4:7 “But the end of all things is at hand; be sober, watchful unto prayer.” We need to use our minds in these end times and have continuous prayer. We need to pray every day just as we eat food every day. The spiritual man needs food just as the physical man does.
Eph 5:15-17 “15 Be very careful how you walk, not as unwise but as wise, 16 redeeming the time, because the days are evil. 17 Therefore do not be unwise, but understand what the will of the Lord is.” We need to be mindful of our behavior after leaving the worship service. We should not just be good during church services. Many servants of God are receiving revelations that the rapture of the church is imminent. We need everything we do to be meaningful for our eternity and our destiny. We must realize that our citizenship is not here but in heaven. Philippians 3:20 “For our citizenship is in heaven, and from it we eagerly await a Savior, the Lord Jesus Christ.” It is not a sin to think about life on earth, but let us not forget that our citizenship is in Heaven. Remember to ask yourself where you will live after this life.
Col 3:1-3 “1 If then you have been raised with Christ, seek those things which are above, where Christ is, seated at the right hand of God. 2 Set your minds on things which are above, not on things which are on earth. 3 For you have died, and your life is hid with Christ in God.” After leaving the church service, do you ever think about what our life will be like in Heaven? Do you think about God’s work? Or maybe you only think about how you will make money? If you have a worldly mindset, you are making God have no reason to bless you. You must surpass an unbeliever.
1 The 5:21 “test everything; hold fast what is good.” Measure your life, learn to put yourself on the scale. Ask yourself if you find time to think about the Kingdom of God. We need to change, not only during church service but even when we are at home. The apostles were not people who owned many worldly things, but they were filled with joy. Their joy was not in things but in the Lord. Philippians 4:4 “Rejoice in the Lord always; again I will say, Rejoice.” When Satan discovers that his temptations put you in danger, he will persecute you greatly. Satan surrenders when he realizes that even when he torments you, you are still doing God's work.
MWISHO UMEKARIBIA, TUWE NA AKILI
Tunaona kama miaka elfu mbili tangu aje Bwana Yesu duniani, ni mingi sana. Kumbe ni sawa na siku mbili tu Kwake.
1 Petro 4:7 “Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.” Tunatakiwa kutumia akili zetu katika nyakati hizi za mwisho na kuwa na maombi endelevu. Tunatakiwa kufanya maombi kila siku kama tunavyokula chakula kila siku. Mtu wa rohoni anahitaji chakula kama alivyo mtu wa mwilini.
Efe 5:15-17 “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” Tunatakiwa kuwa waangalifu kuhusu mienendo yetu baada ya kutoka ibadani. Tusiwe wazuri tu nyakati za ibada kanisani. Watumishi wa Mungu wengi wanapata ufunuo kwamba unyakuo wa kanisa uko karibu. Tunatakiwa kila tunachokifanya kiwe na maana kwa ajili ya umilele wetu na hatima yetu. Lazima tutambue kwamba uraia wetu sio wa hapa bali ni wa mbinguni. Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.” Sio dhambi kuwaza maisha ya hapa duniani, lakini tusisahau kwamba kwetu ni mbinguni. Kumbuka kujiuliza kwamba baada ya maisha haya utakaa wapi.
Kol 3:1-3 “1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.” Hivi baada ya kutoka ibada, kuna muda unatafakari kuhusu maisha yetu yatakavyokuwa huko Mbinguni? Je, unawaza kuhusu kazi ya Mungu? Au pengine unawaza tu jinsi utakavyopata pesa? Kama unawaza kama watu wa dunia hii, unamfanya Mungu akose sababu ya kukubariki. Lazima umzidi mtu ambaye sio muumini.
1 The 5:21 “jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.” (test everything; hold fast what is good). Pima maisha yako, jifunze kujiweka katika mizani. Jiulize kama unapata muda wa kuwaza kuhusu Ufalme wa Mungu. Tusibadilike muda wa ibada peke yake bali hata tukiwa nyumbani. Mitume hawakuwa watu waliomiliki vitu vingi vya dunia hii lakini walijawa na furaha. Furaha yao haikuwa katika vitu bali katika Bwana. Wafilipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.” Shetani akigundua kwamba akikubana mahali unakata tamaa, atakutesa sana. Shetani ananyosha miko anapogundua kwamba hata akikutesa unazidi kufanya kazi ya Mungu.
Dr. Lawi Mshana, +255 712-924234, Tanzania