Ticker

6/recent/ticker-posts

Business or Project Startup No. 3: Declare it as God’s work (Uanzishaji wa shughuli au mradi Na 3: Itangaze kama kazi ya Mungu)

Video link: Na 3. Tangaza shughuli yako kama kazi ya Mungu

Business or Project Startup No. 3: Declare it as God’s work (Uanzishaji wa shughuli au mradi Na 3: Itangaze kama kazi ya Mungu)

Declare your business as God’s work. Don’t see it as your own work. Altar ministry is not just preaching; it is also doing your business, then coming to church and giving offerings and tithes. So speak blessings for your business. It is God’s work because you have obeyed His command not to be lazy. Say to God, ‘This business is Yours, the Provider. So You (my Lord) will bless it because it is Your work.’ You can have the courage to ask God for customers so you can be a blessing to His work. By doing so, you are giving God a debt to bless you. You cannot pronounce that if you do not use the income from that business to give to God. From now on, speak blessings for your business because even the children you raise belong to God. So never distinguish the work that you do at home from the ministry you do when you go to church.

Uanzishaji wa shughuli au mradi Na 3: Itangaze kama kazi ya Mungu

Tangaza shughuli yako kama kazi ya Mungu. Usiione kama kazi yako binafsi. Utumishi wa madhabahuni sio kuhubiri peke yake bali hata wewe unayefanya kazi yako na kisha kuja kutoa sadaka na zaka. Hivyo itamkie mema na kuitabiria kazi yako. Ni kazi ya Mungu kwa vile umetii agizo lake la kutokuwa mvivu. Mwambie Mungu, ‘Hii shughuli ni Wewe umenipa hivyo utaibariki kwa vile ni kazi Yako.’ Unaweza kuwa na ujasiri wa kumuambia Mungu nipe wateja ili upate sadaka kwa ajili ya kuibariki kazi Yako. Ukifanya hivyo unampa deni Mungu ili akubariki. Huwezi kutamka hivyo kama tu hutumii pato la shughuli hiyo katika kumtolea Mungu. Kuanzia sasa tamka baraka kwa ajili ya shughuli yako kwa vile hata watoto unaowalea ni wa Mungu. Hivyo usitofautishe kazi yako unayofanya nyumbani na kazi ya Mungu unayofanya ukienda kanisani.

Dr Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania