SHIRIKIANA NASI MWAKA 2025 (video)
KARIBU USHIRIKIANE NASI KUIHUDUMIA JAMII MWAKA 2025
Unaweza kujitolea ujuzi wako rasmi au usio rasmi katika kushirikiana na sisi.
Unaweza kushirikiana na sisi kwa kujitolea ujuzi wako, fedha zako, kuazima vifaa au eneo lako, kutuunganisha na fursa nk
Kujitolea kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata marafiki wapya, ujuzi mpya, utoshelevu katika maisha, kuuza ujuzi wako, kutoa shukrani kwa jamii, kukabili msongo wa mawazo na kubarikiwa na Mungu.
Tunatoa huduma kwa watoto, vijana na familia zinazoishi mazingira hatarishi ili kuwajengea uwezo washinde umasikini, utegemezi na uhatarishi.
Karibu sana na Mungu akubariki.
Dkt. Lawi Mshana, Mkurugenzi Mtendaji, Beyond Four Walls, +255712924234, Tanzania