Ticker

6/recent/ticker-posts

18. Anointing is not only for spiritual ministries (Upako sio kwa ajili ya huduma za kiroho pekee)


 Video: Na 18 Upako sio kwa ajili ya huduma za kiroho pekee

18. Anointing is not only for spiritual ministries

(Upako sio kwa ajili ya huduma za kiroho pekee)

Isa 10:27 “It shall come to pass in that day That his burden will be taken away from your shoulder, And his yoke from your neck, And the yoke will be destroyed because of the anointing oil.” Anointing can destroy the burden on your shoulder and the yoke around your neck. Perhaps you complain and suffer because you do not know that you have been given authority. Anointing is not just for altar services. We want your anointing to operate in your home too. Anointing is not location-specific. Anointing can operate in the office, the market, and the farm. It is only your problem to limit your anointing to preaching the Gospel only. That is why neither your farm nor your business is anointed. You need to regard your business as God's work.

Please send your love gift to support this ministry. +255 712924234 or CRDB Bank; Account Name: Lawi E. Mshana; Account Number: 0152219784300; Swift Code: CORUTZTZ

Isa 10:27 “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.” Upako unaweza kuharibu mzigo uliokulemea begani na nira uliyofungwa shingoni. Pengine unalalamika tu na kuteseka na hujui kwamba umepewa mamlaka. Upako sio kwa ajili ya huduma za madhabahuni tu. Tunataka upako wako utembee hadi nyumbani kwako. Upako hauchagui eneo. Upako unaweza kutembea hadi ofisini, sokoni na shambani. Ni wewe mwenyewe umeuwekea mipaka kwamba uwe upako wa kuhubiri tu Injili. Ndiyo maana hakuna upako kwenye shamba lako wala kwenye biashara yako. Unatakiwa kuiona shughuli yako unayofanya kwamba ni kazi ya Mungu.  

Bofya video usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.

Dr. Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania