Ticker

6/recent/ticker-posts

No. 4. The finished work of Christ (Kazi aliyomaliza Kristo msalabani) – Online Conference

Video link:  Na 4. Kazi aliyomaliza Kristo msalabani

No. 4. The finished work of Christ (Kazi aliyomaliza Kristo msalabani – Online Conference

The accuser no longer has legal rights. No legal accusation from the devil. 

The accuser no longer has legal rights against us. So you have no reason to live in fear. You need to know who you are. You are seated with Christ in the spiritual realm. You reign with the Lord Jesus. As we spend more time with the Lord, we are promoted and gain greater authority. Even Jesus’ disciples were given authority over demons and all kinds of diseases when they spent time with him. Even though you are saved, some things don’t happen because you haven’t had enough time to spend with the Lord. Remember that even the Lord Jesus spent some time and was declared to be the beloved Son in whom God is well pleased. It is important to know the level of your authority now. 

Rev 12:10 “And I heard a loud voice in heaven saying, Now is come salvation, and strength, and the kingdom of our God, and the authority of his Christ: for the accuser of our brethren is cast down, which accuseth them before our God day and night.”

If you pray, you reach the heavenly court. Satan is there as your accuser. However, when we express ourselves instead of lying and ask for forgiveness, God has mercy on us even if we have done wrong. 

Kazi aliyomaliza Kristo msalabani

Mshitaki hana tena mashitaka yenye nguvu ya kisheria kuhusu sisi. Kwa hiyo huna sababu ya kuwa na maisha ya hofu. Unatakiwa kujitambua wewe ni nani. Umeketi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho. Unatawala pamoja na Bwana Yesu. Tunavyozidi kukaa na Bwana tunapandishwa vyeo na kupata mamlaka kubwa zaidi. Hata wanafunzi wa Yesu walipewa mamlaka juu ya mapepo na magonjwa ya aina zote walipokaa naye kwa muda fulani. Ingawa umeokoka, kuna vitu havifanyiki kwa vile hujapata muda wa kutosha kukaa na Bwana. Kumbuka hata Bwana Yesu alikaa muda fulani ndipo akatangazwa kwamba ni Mwana mpendwa ambaye Mungu anapendezwa naye. Ni muhimu kutambua kiwango cha mamlaka yako kwa sasa.

Ufu 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.”

Ukiomba unafika kwenye mahakama ya mbinguni. Shetani anakuwepo kama mshitaki wako. Hata hivyo tunapojieleza vizuri bila kudanganya na kuomba msamaha, Mungu anaturehemu hata kama tulikosea.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania